Wafugaji Pwani · Utafiti wa mahitaji
Umoja Wetu,
Nguvu Yetu.
Maendeleo ya Ufugaji
Dodoso la utafiti wa mahitaji ya wafugaji wa ng’ombe wa Ukanda wa Pwani ya Tanzania
Kuelekea kuanzishwa kwa umoja/chombo cha wafugaji
Ndugu Mfugaji, tunatarajia kuanzisha Umoja/Chombo cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Ukanda wa Pwani ya Tanzania na mikoa jirani kwa lengo la kuunganisha wafugaji, kutetea maslahi yao, kuboresha uzalishaji, kupunguza gharama za ufugaji, kuongeza thamani ya mazao na kutafuta masoko yenye faida.
Kabla ya kuanzisha umoja/chombo hicho, tunafanya utafiti ili kufahamu changamoto, mahitaji na matarajio ya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa na nyama. Japo ukanda wa majaribio ni Ukanda wa Pwani, lengo ni kuwafikia wafugaji wote nchini Tanzania. Tunawakaribisha wafugaji wote walio tayari kutoa maoni na kuangalia uwezekano wa kujiunga kadri utaratibu utakapokuwa tayari.
Ushiriki ni wa hiari. Taarifa utakazotoa zitatumika kwa madhumuni ya utafiti. Taarifa binafsi hazitatangazwa bila ridhaa yako.
Umoja Wetu, Nguvu Yetu, Maendeleo ya Ufugaji.